Duration 6:51

MKUU WA MKOA WA ARUSHA RC KIMANTA AONDOKA MONDULI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

553 watched
0
7
Published 2020/06/25

MKUU WA MKOA WA ARUSHA RC KIMANTA AONDOKA MONDULI KWA MAFANIKIO MAKUBWA. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Iddi Kimanta amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Monduli na Wananchi kwa kumpa ushirikiano Mkubwa kipindi akichokuwa Mkuu wa wilaya ya Monduli kwa kipindi chote alichokuwa anatekeleza majukumu yake kama mkuu wa wilaya ya Monduli. . . . Ameyasema hayo wakati akimkabidhi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya ya Monduli Mh.Acp.Edward Jotham Balele ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Monduli, kabla ya uteuzi huo nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mh.Rc Kimanta ambaye kwa sasa ni Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha, pia akizungumza na wafanyakazi wote katika ukumbi wa Halmashauri amewashukuru sana na ametambua mchango wao Mkubwa waliompa kipindi chote na kuwaomba waendelee kudumisha ushikamano huo kwa viongozi wao na kuheshimiana wakati wote huku wakiendelea kuchapa kazi kwa bidii. . . . . Pia Mkuu wa mkoa Mh.Kimanta ametoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Stephen ulaya Mkuu mpya wa wilaya ya Monduli kuenda kusimamia kumalizia Ukamilishwaji wa Miundombinu ya Shule za Sekondari, kwani tayari wananchi wameshachanga kiasi cha Tsh milioni 400 ambazo zipo tayari benki. Amemwambia Afisa manunuzi kutokuchelewesha ufanyaji wa manunuzi, lengo ni kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa nguvu kubwa za wananchi ili atakapo fanya ziara bada wiki mbili akute ujenzi unaenda kasi. Amemtaka pia Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Afisa Biashara wilaya ya Monduli kuhakikisha wanashirikiana kuongeza kasi ili kumaliza vitambulisho vya wajasiriamali vilovyotolewa na Mheshimiwa Raisi John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya wajasiriamali wadogo. RC KIMANTA RC ARUSHA Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Leo 25/06/2020 Monduli ELIFURAHA RAPHAEL(KABURU).

Category

Show more

Comments - 0