Duration 2:24

WACHAGA WANAPENDA MAGENDO WAZEE WACHARUKA NA KAULI HIYO

123 watched
0
0
Published 2021/11/29

BAADHI ya wazee wa kabila la Wachagga wamelaani kauli ya Mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei aliyoitoa hivi karibuni Bungeni ya kuwa Wachaga ni watu wanaopenda Magendo huku wakimtaka kuomba radhi na kuifuta kwenye kumbukukumbu za Bunge. Mbali na hatua hiyo Wazee hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao Raymnd Mushi wamekiomba chama kilichompa dhamana ya kuogombea ubunge katika jimbo la Vinjo kumchukulia hatua za kinidhamu kwani aliyoyasema Bungeni si yale waliyomtuma. Katika kipindi cha maswali na majibu wakati wa kikao cha bunge Dkt Kimei alisema “Jimbo la Vunjo mheshimiwa Spika ni jimbo lililo mpakani na majimbo yaliyompakani yanakuwa na changamoto tofauti kidogo kwa mfano Magendo,unajua wachaga wanavyopenda Magendo ,dawa za kulevya zinaingia harafu kuna kuwa na uhamiaji haramu” “Kwa hiyo kuna umuhimu na tunaomba serikali ituhakikishie kwamba itachukua hatua gani ili kimarisha ulinzi kwenye vituo vya polisi na kuwaongeza polisi pamoja na bajeti kwa sababu wanahitaji kuchukua hatua haraka mambo yale yanapotokea.”aliongeza Dkt Kimei . #Cloudsdigitalupdates

Category

Show more

Comments - 0