Duration 8:2

WALIOONDOLEWA NA VYETI FEKI WAPEWE HAKI ZAO-MBUNGE MRISHO GAMBO

14 953 watched
0
65
Published 2021/04/24

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ameitaka Serikali kuwaangalia watumishi wa umma waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki kwa kuwapa mafao na kiinua mgongo chao. Mbunge huyo ametoa ombi leo Ijumaa Aprili 23, 2021 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka 2021/2022 Gambo amesema Serikali ilifanya zoezi muhimu na nyeti la kufanya uhakiki vyeti vya watumishi wa umma na liliwasaidia kufanya usafi kwenye sekta ya utumishi wa umma kwa kuwaondoa wasiostahili lakini haikuwalipa stahiki zao. Amesema anakumbuka kuwa taarifa ya mwisho ya Serikali ilisema 511589 ambao ni sawa na asilimia 96.71 walihakikiwa lakini 14,409 walibainika kuwa na vyeti feki na watumishi 1907 walikuwa bado hawajapeleka uthibitisho wa vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa.

Category

Show more

Comments - 84
  • @
    @mariammpangalala84233 years ago Mungu akubariki sana Mrisho Gambo kwa kuwakumbuka wananchi hawa
  • @
    @kisetukumbuael18393 years ago Unafiki huu utawaacha lini viongozi ,mnanifanya nikose imani na uongozi huu na njia mnaanza kupoteza 4
  • @
    @rosetreffert67273 years ago Magufuli tutakukumbuka Sanaa 🙏🙏❤❤ WANAFIKI WAMEZIDI HADI KICHEFUCHEFU
  • @
    @peternichoraus59833 years ago Mmmmh huu ndy unafiki wenyew yetu macho 4
  • @
    @peterlawrence86183 years ago Mbunge wangu eniumiza Sana kwapumba isiokufanana wewe cheti chako kingenunuliwa hapo ulipo ungekuwepo niwangapi wamesomeshwa kwa shida wanafikia kuhitimu wanfauru ,wanaonekana wamefel wenye nafasi zao wanawafaulishia watu wao! Je walioibiwa vyeti vyao hawana familia zinazowategemea? Wakat wanalipwa mishahara walio ibiwa nafasi zao familia zao zinatunzwa na nani? Eh Mungu mlaze mahali pema pepon jpm oh! Bado tunaumia kwakuondoka kwako . Huu ujinga usinge uvumilia ...
  • @
    @rahmahersi21163 years ago Wana Bungeni
    Fluet swahili..between
    WALAKA NA WARAKA.
    CORRECTION PLS.
  • @
    @magrethpoulpoul85853 years ago Watu mnakera unafiki huu jmn. Naamin jpm anazoom2 anaishia kutikisa kichwa na kujisemea hiiiiiiiiiiiiii.pumzk kwa amn jpm tunakupenda bdo tunakukumbka💔❤🙏 1
  • @
    @suzanakameta55963 years ago Wewe ni mnafiki, kwa nini usiseme wakati Magufuli yupo? Acha hizo. 2
  • @
    @loner_wolf3 years ago Mbunge anaonyesha upumbavu wake. CHETI KISICHO HAKI KINAKUWAJE NA MADAI YA HAKI... Yaan unasimama kutetea watu ambao walitakiwa kuwa jela sasa hivi.... Ukumbuke hilo, ujue tu washasababisha kufelisha watoto kibao wa nchi hii just kwakudanganya wao ni walimu ilhali ni njaa tu zinawasumbua..... ...
  • @
    @bmajesky633 years ago Point Sana Mkuu kweli walifanya kazi Tena walijituma kuliko hao wenye vyeti Vizuri So watazamwe kiubinadamu Hapo ilifanyika Dhuruma Kubwa sana 4
  • @
    @isayangonyani26783 years ago Point Sana mkuu,niwazi serikali ilichangia hivyo wapewe halo zao komsingi.kwa sababu walifanya kazi. 1
  • @
    @claudbusumilo39793 years ago Gambo wewe nikichwa unaongea point tukila wakati
  • @
    @princessmallya84393 years ago Big point big fact
    Na pia wenye vyet fek ndo walikua wanfanyakazi bila ya dharau wala nyodoo hata ukimpangia kazi bila mapumziko watafanya tuu coz wanajuaa umuhimu wa hyo kazi
    Ila sasa hawa wenye vyet orijino jaman wanajisahau sanaa full poz zarau nyingi hadi wanaboaa.....mnyonge mnyongen lakn haki yake mpeniii.....amen
    ...
    1
  • @
    @jumakapilima56743 years ago Kwa baadhi ya hoja hizi za waheshimiwa (vyeti feki), ndio maana nasema chondechonde mama yetu awe makini maana miruzi ishakuwa mingi , mtangulizi wako aliiweza nchi hii kwa kuwa hakuwa anasikiliza miruzi hiyo,,,,,,,,kwa maana ninavyojua forgery (vyeti feki) unapaswa kushitakiwa mahakamani na ukafungwe!! ...
  • @
    @alfredkalaba16143 years ago Enzi za Mhe. Magu asingesema hayo. Kweli unafiki mwingii
  • @
    @frankrevelian69193 years ago unafiki tu, hamna hoja hapo... watu wana vyeti halali wamekosa nafasi zao, serikali imeingia hasara kwa sababu ya wafanyakazi ambao hawana ujuzi, alafu leo eti tuwalipe... kutowapeleka mahakamani ilikuwa busara na iishie hapo... hatutaki unafiki... waliokosa izo nafasi na wana sifa halali utawalipa nn... ...
  • @
    @dedrickgosso87113 years ago Unazunguka sana be strait au ndo ugeni bungeni
  • @
    @husseinyusuph54583 years ago Wapewe haki zao kivipi wakat wamewakatili wenye vyet vyao kukosa kazi
  • @
    @paschalmartin12733 years ago Yaaani una watetea vyeti feki ambaye kufoji cheti ni kosa kisheria alitakiwa ashtakiwe wewe unasema alipwe kweli duuh! Hii siasa za kinafiki
  • @
    @frankmakomba3783 years ago Wabunge wengine wapo tu; Bungeni wanasimama kutoa hoja ili waonekane kwa wapiga kura wao.
    Mbunge anasimama kutetea waliofoji vyeti. Kuna Dokta wa meno alikuwa amefoji cheti cha udaktari,
    badala ya kung-oa jino lililo bovu, akang-oa jino zima jirani yake ; Pia si walikuwa wanapata mishahara, likizo .....
    ...
  • @
    @nebuchadne33ar3 years ago Nikafikiri ataongelea wale ambao waliambiwa vyeti vyao ni feki lakini vilikuwa sahihi
  • @
    @restkalemile52743 years ago acheni unafik.... mbona magufuli akiwa hai hukulizungumza...... mnajidai mnajali maslah ya watu lakin sivyo mmejaa ubinafs na unafki 4
  • @
    @josiamwambona27853 years ago Jina feki sasa feki teeena bro hauko serious au umekosea
  • @
    @rosetreffert67273 years ago Wewe Mbunge UNAONGEA UPOYOYO YAANI WAMEIBA VYETI NA KUZIBIA NAFASI ZA WENYE HAKI !!!ACHA KUJIPENDEKEZA NA UNAFIKI MTUPU , TOA KWENYE POSHO YAKO MNAPATA HELA NYINGI
  • @
    @JohnJuma3 years ago Cheti feki, haki inatoka wapi? Wanafaa kuregesha pesa zote walopata
  • @
    @davidzacharia61443 years ago Wewe mbunge acha unafiki tengeneza CV iwe ya msingi usiwe mnafiki. Ukiwaunaongea ili mradi wapiga Kura wako wamekusikia punge linalokuja utarisikia tu
  • @
    @karyori693 years ago Vp waliokosa nafasi hizo kwa sababu ya udanganyifu ya waliofukuzwa na walikuwa na vyeti halali? hawapaswi kulipwa fidia pia? Huu unafiki aisee JPM huko alipo atakuwa anasikitika!
  • @
    @nicholausmasese63373 years ago WW NI MLEZI MZURI WA PIMBI TARAJIA MKIA
  • @
    @homeofvideos88933 years ago Aisee watu kama hawa wanatakiwa wararuliwe na radi kwanini asingemwambia hayo aliyewatoa hao wenye vyeti feki anajua hao wenye vyeti feki walizuia ajira za wenye vyeti halali wangapi au kisa yeye anapata hela kwa kuclick ndo maana anaongea shit. Acha unafiki usijifanye huwezi kuwa mtu wa ndio wakati ulikuwa mtu wa ndio wakati wa mzee. Ningekuwa mchawi ningewamaliza wapuuzi wote kama hawa sinaga uvumilivu wa ujinga et ...
  • @
    @happymrema67283 years ago Makoful angekuwepo usingeingea huo upuuz
  • @
    @chugachugambuli88793 years ago Huyu jamaa naye pumba kabisa , ndo matunda ya kupenda sifa haya ili uonekane mwema ...unaanzaje kutetea vyeti feki wakati wasomi wamejaa mtaani
  • @
    @magrethpoulpoul85853 years ago Usiamin kila anayesem nip nyuma yko. Onen ssa jpm amegeuka amejikuta yup pke yake na mung wake
  • @
    @davidzacharia61443 years ago Nyie wabunge mnajisahau Sana hamko kuwatetea wananchi mmeingia kula tu Bora muwe mnafanyiwa usahili kamili siokubebana
  • @
    @neziajoseph97263 years ago Haki gani na watu wameforge vyeti? Sasa nyie hii itakua nchi ya kizombi sana,Yani mtu kaforge cheti tena yy ndo kakuibia halafu umpe haki gani?au ww ndo unapaswa umshtaki 3
  • @
    @seifmohamed8363 years ago Ulipokuwa mkuu wa mkowa WaArusha kwanini hukumwambia magufuli hivo kama unasema ya ukweli
  • @
    @francescorutinwa5023 years ago Haki ipi sasa? Si mishahara walikuwa wanapokea au? Unajua kwenye kazi hizi kuna vigezo na masharti kuzingatiwa sasa mtu kuajiriwa n kufanya kazi kwa njia za magendo huku ukiwa unaufahamu unachofanya hicho ni sawa na ku take risk tu hapo ni kutegemea mawili siku likibumburuka lazima uliwe kichwa au upate salia mtume tu.Sasa hpo unadai nin sasa jman? Mhe. Gambo hao unaowatetea ndo hao waliokuwa wamekalia nafasi za ajira za watu waliosotea kwenye elimu kwa muda mrefu bila ajira. Nchi yetu bado masikini inaendelea huwezi kubeba kila mtu huo ndo ukweli na hizo gharama nani atazibeba hpo? ...
  • @
    @mtakatifuelisha81653 years ago Huyu jamaa ni pumba kabisa , unafiki mtupu
  • @
    @blueeyes59523 years ago Upumbavu pekee, mtu iko na vyeti feki serikalini , amefukuzwa unasema eti walipwe na serikali, si uwapatie mshahara wako ? Wote wangetiwa gerezani kwa ku fanya vyeti bandia kwa jina la serikali. Wabunge wa wajinga sana wanaongeya bila kufikilia njo maana magufuli alifukuza ujinga huu ...
  • @
    @dismasstanslaus59853 years ago Safi Coz inchi niyakwetu we hv being enjoy national cake kwasabu kuna wanna kula kilaini huko na uchumi huko serikalin wakati nchi ni ya kwetu sote ndomanaa mi namkubali Sana mama sami anaakili nyingi msimuone vile yule mama ni mungu lazma ambariki usibague watoto wako hata kama moja nimjinga mwingine anaakili wote si watoto lazma wapate haki za baba yao na kila moja arizike that is the national cake au nasema uongo jmn?? ... 1
  • @
    @manasesana14203 years ago Hii Tanzania ina wabunge tope kweli! Yani wapewe mafao? Hao watu wangetakiwa wafungwe. Walichukua nafasi za watu wenye uwezo, wametoa huduma chini ya kiwango, wameiingiza serekali hasara, wamekatisha tamaa wazazi waliosomesha watoto wao, wamekatisha tamaa watu waliosoma na wenye ujuzi uliohitajika, na mengine chungu nzima! Shame on you gambo. ...
  • @
    @husseinyusuph54583 years ago Wapewe haki zao kivipi wakat wamewakatili wenye vyet vyao kukosa kazi