Duration 35:30

TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC: FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - )

862 900 watched
0
1.6 K
Published 2018/12/03

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, leo wamefanya kweli Jijini Mbeya kwa kuichapa Tanzania Prisons jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Wenyeji Tanzania Prisons ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Jumanne Elifadhili, penati ambayo ilizua tafrani na kupelekea wachezaji watatu wa Yanga kupata kadi za njano. Yanga waliingia kivingine kipindi cha pili na kusukuma mashambulizi ya kasi hasa baada ya kuingia wachezaji wapya Matteo Anthony, Thabani Kamusoko na Amissi Tambe na kupata bao la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penati. SUPER SUB: Amissi Tambwe ameingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Juma Abdul, akasababisha penati iliyosababisha bao la kusawazisha, kisha akafunga mengine mawili dakika ya 85 na 90+2. Timu zote zililazimika kucheza pungufu baada ya Tanzania Prisons kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati, hali ikaonekana si shwari tena uwanjani na kupelekea vurugu ambazo zilizaa kadi nyekundu mbili, yaani moja kila upande. Mara baada ya mchezo wachezaji Mrisho Ngasa na Laurian Mpalile wamezungumza na kuomba radhi mashabiki kwa kitendo walichoonesha, huku Kocha Mwinyi Zahera akimwaga machozi.

Category

Show more

Comments - 255