Duration 35:46

Somo la 3: UMUHIMU WA KUVAA SILAHA ZA MUNGU..NA MCH RAPHAEL KITINE

1 115 watched
0
17
Published 2019/10/13

Efeso 6:11 “…Vaeni silaha zote za Mungu…” Kufungiwa Utayari Tupatao Kwa Injili Ya Amani Efe 6:15 I. UTANGULIZI • Naomba nikukumbushe kuwa mwandishi wa waraka huu kwa kanisa la Efeso, Mtume Paulo amechukua picha ya askari shupavu wa jeshi la kirumi aliyejitosheleza kwakuvaa silaha zote muhimu • Akimfananisha na askari shupavu wa jeshi la mbinguni katika ulimwengu wa roho, aliyejitosheleza silaha zote muhimu katika kupigana na adui shetani. • Je unapenda kuwa askari shupavu wa jeshi la mbinguni? Fuatilia mfululizo wa somo hili na kuchukua hatua za mabadiliko! • Wakati uliyopita katika somo hili, tulijifunza jinsi askari shupavu awezavyo kuitumia dirii ya haki katika kifua chake, katika kujikinga na mishale ya adui. II. SOMO LA LEO i. Ufafanuzi wa somo “…na kufungiwa miguu utayali tupatao kwa injili ya amani…” Efeso 6:15. • Kwa kutusaidia kupata ufafanuzi zaidi wa kuelewa somo letu inabidi tusome neno hilo hilo ktk Biblia tafsri tofauti: • Habari Njema “…na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu…” Efeso 6:15. • New Revised Standard “As shoes for your feet put on whatever will make you ready to proclaim the gospel of peace”…Eph 6:15 RSV. • Inatupasa kutangaza habari njema ya wokovu kama vile ilivyo muhimu kwa askari kuvaa viatu awapo vitani • Kmkm • Hamu ya kutangaza habari Njema, ni hali ya msukumo wa kusema habari ya wokovu wa Bwana Yesu kwa watu wasio amini Mdo 20:24 “…Huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu…” • Mark 16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. ii. Umuhimu wa askari kuvaa viatu awapo vitani • Watu wengi huvaa viatu kama pambo la mwili, lakini ukweli ni kuwa umuhimu wa viatu ni zaidi ya pambo. • Kwa askari wa zamani nawa sasa huvaa viatu vya tofauti na viatu vingine, • venyewe huwa na sehemu ya mbele ngumu sana, soli imara zaidi na tena kirefu kwenda juu. Faida za viatu kwa askari aliyeko vitani ni:- Ili tuweze kuelewa umuhimu wa kuvaa silaha ya kutangaza habari njema ya wokovu, ni vema sasa tujifunze umuhimu wa viatu kwa askari aliyepo vitani tukilinganisha na silaha ya habari njema 1. Kumsaidia asiteleze na kuanguka apitapo katika matope 2Sam 22:37-38, “Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza. 38 Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.” • Hutusaidia tusiteleze na kuanguka tuwapo vitani Zab 73:2 “…Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza. • Silaha kubwa ambayo shetani huitumia kuleta maangamizi makubwa kwa waamini wengi ushawishi Mith 1:10 • Silaha kubwa ya kupambana na ushawishi wa shetani ni injili Yn 5:4-29 2. Kumsaidia kutochomwa na miiba Mith 22:5, Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. • Hutusaidia kusimama imara wakati wa vita tunapochomwa na miiba • Kazi ya miiba kupitia ncha kali huchoma na kusababisha maumivu makali ya mwili • Shetana hutumia silaha ya miiba kuwachoma watu kiroho na kusababisha maumivu makubwa ya roho na mwili 2Kor 12:7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. • Kwa askari ya mbinguni kujikinga dhadi ya miiba shetani itamsadia kutokatishwa tamaa kuendelea na wokovu (Miiba inaweza kuwa maneno makali na matukio ya kukatisha tamaa 3. Kumsaidia Kutoumwa na nyoka wenye sumu Lk 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. • Huwezi kukanyaga nge na nyoka wenye sumu kama hujavaa viatu vya uhakika • Nyoka wenye sumu wanaotamkwa ktk Lk 10:19 ktk ulimwengu wa roho ni nguvu za shetani zilizoachiliwa kwa ajili ya watu Mungu • Nguvu hizo zinaweza kuwa ni mapepo,nguvu za giza n.k • Kupitia injili ya habari njema ya wokovu tunapewa nguvu za kukabiliana nazo.

Category

Show more

Comments - 8